Friday, July 10, 2009

Shughuli Za Ujenzi Wa Madarasa Zapamba Moto


Mwenyekiti wa kijiji cha mabilioni mzee Kimweri(kulia) wakijadili kitu fulani na afisa mtendaji kijiji cha mabilioni mzee masinka muda mchache kabla kikao cha serikali ya kijiji na WDC hakijaanza
Kubwa zaidi ni kujadili hatua iliyofikia ya ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili za walimu.


mwenyekiti wa kijiji mabilioni (kulia) na mtendaji wakisikiliza kwa makini mjumbe akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kufanya ili ujenzi ukamilike kwa haraka kabla ya mwezi wa tisa ili kuthibitishia kua mwakani shule iweze kupokea vijana 160 wa kidato cha kwanza.
kikao hiko kimefanyika tarehe 10 julai 2009




mjumbe akitoa mawazo yake kuhusu ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ambavyo kwa sasa ndio wanaanza msingi







Mh: diwani mzee Mangare katikati akiwa na mtendaji kata ya hedaru kulia na mwenyekiti wa kijiji cha mabilioni kulia wakisikiliza hoja za wajumbe wa serikali ya kiijiji cha mabilioni kuhusu mikakati ya ujenzi wamadarasa ambao unasuasua.
mh: Diwani amemuagiza mtendaji kijiji cha mabilioni kumfikishia mpango kazi wa ujenzi wa madarasa hayo kabla ya tarehe 15 julai 2009 ili ujenzi ufanyike kwa haraka.
Kikao hiko kilifanyika katika moja ya madarasa ya shule ya sekondari Mabilioni.










No comments:

Post a Comment