Tuesday, January 11, 2011

SHULE YAPOKEA VIFAA VYA MAABARA




Shule imepokea vifaa vya maabara vya masomo ya fizikia kemia na baiolojia vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5.


"hili limefanyika leo tarehe 11 january 2011 na ni mpango kabambe unaofanywa na shule hii unaoitwa science revolution(mapinduzi ya kisayasi) na hili lawezekana kutokana na ushirikiano mkubwa uliokuwepo baina ya waalimu wa shule hii na uongozi kwa ujumla.
tumepanga kufundisha sayansi kama vita ili tuone matokeo yetu baada ya shule yetu kuingia kidato cha nne kwa maana vita hii ni ya chinichini ambayo inahitaji silaha za kutosha ili kupambana nayo, na waalimu msichoke kurudiarudia kwa maana hata makanisani na misikitini tunamo abudu wachungaji na mashehe hurudia rudia ili kuwafanya waumini wao wawe karibu na mungu basi nasi naomba turudie rudie mazoezi haya kwa vitendo na nadharia ili tuwawezeshe watoto wetu wawe karibu na sayani, inawezekana ila tujitolee kutimiza wajibu wetu" alisema mkuu wa shule(bwn bakari nyambwiro) kwenye kikao na waalimu wa idara ya sayansi.

No comments:

Post a Comment