Saturday, May 28, 2011
Tuesday, March 1, 2011
Saturday, February 26, 2011
KIKAO CHA BODI
Wajumbe wa bodi, mara baada ya kikao kilichofanyika tarehe 25 feb 2011. kutoka kushoto ni bakari nyambwiro(katibu), kahabi(mwenyekiti),mwl.kisaka(mualikwa), Anna Mwajiwa(mjumbe),Dr. Godson Mangare(M/Mwenyekiti), Magreth juma(Mjumbe) MWl.Josephine machimu(Mjumbe)Ngoye Elieskia(Mjumbe), mtari wa nyuma kuanzia kulia, mzee kileng'a(mjumbe), wales kisaka(mwalikwa), mbwambo(Mwalikwa),Wales Makura(mjumbe) Mwl. aloyce shayo(mwalikwa), Mwl.Erast Patrice(mwalikwa) Mzee dismas Muono(mjumbe)
Tuesday, January 11, 2011
SHULE YAPOKEA VIFAA VYA MAABARA
Shule imepokea vifaa vya maabara vya masomo ya fizikia kemia na baiolojia vyenye thamani ya zaidi ya milioni 5.
"hili limefanyika leo tarehe 11 january 2011 na ni mpango kabambe unaofanywa na shule hii unaoitwa science revolution(mapinduzi ya kisayasi) na hili lawezekana kutokana na ushirikiano mkubwa uliokuwepo baina ya waalimu wa shule hii na uongozi kwa ujumla.
tumepanga kufundisha sayansi kama vita ili tuone matokeo yetu baada ya shule yetu kuingia kidato cha nne kwa maana vita hii ni ya chinichini ambayo inahitaji silaha za kutosha ili kupambana nayo, na waalimu msichoke kurudiarudia kwa maana hata makanisani na misikitini tunamo abudu wachungaji na mashehe hurudia rudia ili kuwafanya waumini wao wawe karibu na mungu basi nasi naomba turudie rudie mazoezi haya kwa vitendo na nadharia ili tuwawezeshe watoto wetu wawe karibu na sayani, inawezekana ila tujitolee kutimiza wajibu wetu" alisema mkuu wa shule(bwn bakari nyambwiro) kwenye kikao na waalimu wa idara ya sayansi.
Subscribe to:
Posts (Atom)