Wednesday, July 22, 2009

uchaguzi wa serikali ya wanafunzi tarehe 17 Julai 2009 na mendeleo ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu







serikali ya wanafunzi pichani. vijana hao wawili ni kaka mkuu kushoto na katibu mkuu kiongozi wa shule picha nyingine ni Mwalimu mrimi (makamu wa mkuu wa shule) akiongea na viongozi.Picha nyingine ni maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu ambao unatarajiwa kukamilika tarehe 10 agost 2009








Tuesday, July 14, 2009

ujenzi wa ofisi ya walimu mara baada ya staff room kua maktaba


wanafunzi wakishusha madirisha kutoka kwenye gari



Fundi akijitahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi ya walimu


Saturday, July 11, 2009



mti huu ulipandwa na mheshimiwa mkuu wa wilaya bw. Marwa alipofanya ziara katika shule hii mwishoni mwa mwezi wa pili 2009. Shughuli za mazingira na upandaji wa miti katika shule hii ni shughuli mama, tayari tumeshapanda miti zaidi ya 1000, ingawa tunakwamishwa na swala la maji kwa ajili ya kumwagilia miti hiyo.



ujenzi wa ofisi ya walimu ukiwa umeshika kasi,ujenzi huo unatakiwa kukamilika kabla ya tarehe 22 julai 2009 ili waalimu wapate mahala pa kukaa na kuandaa masomo baada ya kunyang'anywa staff room yao na kuibatiza kua maktaba na reading room.






ujenzi wa nyumba ya mwalimu umeshaanza na kuta zinapandishwa





hiyo sehemu ya kati ya madarasa mawili ndio tunategemea kujenga ofisi ya walimu ambapo baadae itakua ni ofisi ya taaluma




Huu ni msingi wa madarasa manne na ofisi mbili kwa ajili ya kidato cha kwanza mwaka 2010








.

Friday, July 10, 2009

Shughuli Za Ujenzi Wa Madarasa Zapamba Moto


Mwenyekiti wa kijiji cha mabilioni mzee Kimweri(kulia) wakijadili kitu fulani na afisa mtendaji kijiji cha mabilioni mzee masinka muda mchache kabla kikao cha serikali ya kijiji na WDC hakijaanza
Kubwa zaidi ni kujadili hatua iliyofikia ya ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili za walimu.


mwenyekiti wa kijiji mabilioni (kulia) na mtendaji wakisikiliza kwa makini mjumbe akitoa ufafanuzi kuhusu namna ya kufanya ili ujenzi ukamilike kwa haraka kabla ya mwezi wa tisa ili kuthibitishia kua mwakani shule iweze kupokea vijana 160 wa kidato cha kwanza.
kikao hiko kimefanyika tarehe 10 julai 2009




mjumbe akitoa mawazo yake kuhusu ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ambavyo kwa sasa ndio wanaanza msingi







Mh: diwani mzee Mangare katikati akiwa na mtendaji kata ya hedaru kulia na mwenyekiti wa kijiji cha mabilioni kulia wakisikiliza hoja za wajumbe wa serikali ya kiijiji cha mabilioni kuhusu mikakati ya ujenzi wamadarasa ambao unasuasua.
mh: Diwani amemuagiza mtendaji kijiji cha mabilioni kumfikishia mpango kazi wa ujenzi wa madarasa hayo kabla ya tarehe 15 julai 2009 ili ujenzi ufanyike kwa haraka.
Kikao hiko kilifanyika katika moja ya madarasa ya shule ya sekondari Mabilioni.










Thursday, July 9, 2009

Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu.

shughuli za uchomaji wa matofali zikianza

mtaalamu kutoka wilayani akihakiki jamvi kwenye nyumba ya mwalimu